Jinsi ya kuweka pesa kwa M-Pesa
Kuweka pesa kwenye akaunti yako ya Centrino Capital kutoka M-Pesa huchukua dakika chache. Hakikisha laini yako ya M-Pesa imesajiliwa kwa jina lilelile lililo kwenye akaunti yako ya trading.
Huduma ya M-Pesa kwa wateja wa Kenya inaanzishwa. Hatua zilizo hapa chini zinaonyesha jinsi itakavyofanya kazi. Hadi itakapoanza, weka pesa kwa kadi au uhamisho wa benki kupitia client portal.
Hatua kwa hatua
- 1
Ingia kwenye client portal
Ingia kupitia client.centrinocapital.com na ukamilishe uthibitisho wa akaunti kama bado hujafanya hivyo.
- 2
Chagua Deposit, kisha M-Pesa
Chagua akaunti ya trading unayotaka kuwekea pesa na uchague M-Pesa kama njia ya malipo.
- 3
Weka kiasi na namba yako
Weka kiasi kwa KES na namba ya Safaricom iliyosajiliwa kwa jina lako.
- 4
Thibitisha kwenye simu yako
Ujumbe wa M-Pesa utatokea kwenye simu yako. Hakikisha mpokeaji ni Centrino Capital, kisha weka PIN yako ya M-Pesa.
- 5
Angalia salio lako
Utapokea SMS ya M-Pesa na barua pepe. Salio lako la trading litaongezeka malipo yakishathibitishwa.
Inachukua muda gani?
Malipo mengi ya M-Pesa huingia ndani ya dakika chache. Yanaweza kuchelewa mtandao ukiwa na msongamano au malipo yakihitaji kukaguliwa na mhudumu. Salio lisipoongezeka baada ya saa moja, wasiliana na huduma kwa wateja ukiwa na code ya uthibitisho ya M-Pesa.
Vidokezo vya kulinda pesa zako
- Weka pesa kupitia client portal pekee. Centrino haitakuomba kamwe utume pesa kwa namba ya mtu binafsi.
- Hakikisha jina la mpokeaji kwenye ujumbe wa M-Pesa kabla ya kuweka PIN.
- Hifadhi SMS ya uthibitisho ya M-Pesa hadi pesa ionekane kwenye akaunti yako.
- Withdrawals hurudishwa kwa njia ya malipo iliyosajiliwa kwa jina lako mwenyewe.
